Imewekwa: 19th November, 2018
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) inawakumbusha wateja wake na wananchi wote kwa ujumla masuala muhimu kama ifuatavyo:
1.
Wateja wahakikishe
wanalipa Ankara/Bili zao za maji ndani ya siku thelathini baada ya kupata
Ankara za maji. Malipo ya Ankara za maji yanafanyika kwa kutumia mfumo wa
Kielektroniki wa Malipo wa Serikali (GePG) kwa kutumia njia mbalimbali ambazo
ni: mitandao yote ya simu, mabenki na mawakala wote wa mabenki popote pale
Nchini.
2.
Kuwapo kwa
promosheni ya kurejesha wateja waliositishiwa huduma ya majisafi kwa
malimbikizo ya madeni ya kabla ya tarehe 01 Septemba 2018. Wateja hao
wanatakiwa kufika ofisi za DUWASA ili wapatiwe utaratibu wenye unafuu wa namna
ya kulipa madeni yao mwisho ni tarehe 30 Novemba 2018.
3.
Wateja/Wananchi
wenye mashaka na maunganisho ya majisafi na vilevile kwa wananchi ambao
wanatumia huduma ya majitaka bila kuilipia wanahimizwa kujitokeza ili uteja wao
uweze kuhalalishwa bila ya kulipa TOZO yoyote mwisho ni tarehe 30 Novemba 2018.
4.
DUWASA imefungua
ofisi ya mwito wa simu kwa wateja (Call Centre) kwa wateja kupiga simu kwa
kutumia mitandao yote BURE kwa nambari 0800110078 ambayo inapokea taarifa
mbalimbali kutoka kwa wateja. DUWASA inaomba sana wananchi kuitumia huduma hii
muhimu.
Wananchi
wanakumbushwa pia kuwa malipo yote kwa DUWASA yanafanyika kwa njia rasmi ambazo
zimeainishwa katika tangazo hili na kamwe fedha taslimu asipatiwe mtumishi au
mtu yeyote nje ya mfumo rasmi wa malipo wa Serikali. Aidha huduma zote kama
vile maunganisho ya majisafi na majitaka, marejesho ya maji kwa waliositishiwa,
matengenezo ya mabomba na nyinginezo zinatolewa na watumishi ambao wamepangiwa kufanya
kazi hizo. Hivyo, Wananchi wanakumbushwa kufuata taratibu za kupata huduma na
kamwe MAKANJANJA wasitumike kwa kazi za DUWASA.
Tangazo hili limetolewa na:
MKURUGENZI
MTENDAJI
DUWASA